DOGO JANJA KUTIMULIWA MTANASHATI
Hatimaye
Dogo Janja ametimuliwa rasmi Mtanashati Entertainment kwa kile Ostaz
Juma alichokidai kwamba Dogo Janja hana nidhamu,kukataa kusoma Shule na
kutokuenekana nyumbani mara kwa mara.
Huu ndio ujumbe wa Ostaz Juma Baada ya kuzungumza na mtandao wa Bongo 5 leo Octoba 23 2013
Nimemfukuza Dogo Janja kwasababu hana Heshima,amekimbia
Nyumbani,anakoishi sikujui,nimemtafutia Shule amekataa kusoma yaani kwa
kifupi simuelewi na mimi ni mzazi ambaye nimekabidhiwa kumlea.Kwa hiyo
amenishinda namrudisha kwa wazazi wake
Kwa upande wa Dogo
aliulizwa na kusema hivi 'Ostaz ana matatizo yake,naye ni binadamu kama
binadamu wengine kwa hiyo mimi nasema amenifukuza ila sio kwasababu ya
kuvuta Bangi wala sijakataa Shule.Ningependa tuliache hili Swala mpaka
tutakapokutana Kifamilia ndipo tutajua sababu aliyonifukuza ila sio hizo
alizozitaja'Alisema Dogo Janja
No comments:
Post a Comment