Monday, 11 November 2013

NYAWANA KAISI AFARIKI DUNIA

Nyawana Fundikira (Malkia wa Kinyamwezi) amefariki leo mchana nyumbani kwake alipokuwa akiishi na mumewe Kaisi baada ya kuzidiwa na Malaria kali, na Baadaye mwili ulipelekwa Mwananyamala Hospitali. Nyawana alikuwa muimbaji wa taarabu lakini pia ni mtangazaji wa kipindi cha AMBAA NA MWAMBAO kila siku ya jumamosi kuanzia saa Tisa Mchana  na jumapili kuanzia saa kumi na moja jioni hadi saa tatu usiku. PASSION FM DAR ES SALAAM.
Msiba upo kwa baba yake maeneo ya Magomeni kwa Bibi nyau karibu na msikitini, Mwili wa marehemu utasafirishwa kesho jioni kwaajili ya mazishi nyumbani kwao Tabora alipozaliwa na kukulia Marehemu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...