Monday, 28 October 2013
BABA MZAZI WA MTANGAZAJI DIVA WA CLOUDS FM NDIYO RAIS MPYA WA TFF
Baada ya uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Water front kumpata Rais mpya wa TFF kati ya Athumani Nyamlani na Jamal Malinzi, hatimaye TFF imepata Rais mpya ambaye ni Jamal Malinzi.
Mashuhuda waliokuwepo hapo ukumbini wanasema kwamba mpinzani wa Jamal Malinzi alitoka kabla ya utaratibu mzima wa uchaguzi kuisha. Baada ya matokeo kutangwaza Jamal Malinzi alimzidi kura Athumani Nyamlani na hatimaye kupata nafasi ya kumrithi Leodigar Tenda.
Kama ulikuwa hujui ni kwamba Rais huyu wa TFF Jamal Malinzi ndiyo baba wa DivaLoveness wa Ala za Roho ya Clouds FM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment