Sunday, 27 October 2013

WEMA SEPETU AFIWA NA BABA YAKE MZAZI

Kupitia www.yusraction.com tunawapa taarifa zilizotufikia kuwa Miss Tanzania 2006, Wema .A. Sepetu  Amefiwa na Baba yake mzazi, Balozi Isaac Abrahamu Sepetu. Marehemu Amefariki jijini Dar-es-salaam katika Hospitali ya TMJ  na Mipango ya mazishi inafanyikia nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar.  Pole Wema


Info zinasema kuwa Mzee Isaac Sepetu alikuwa mgonjwa kwa muda wa miezi kadha hivi karibuni na amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kiharusi na kisukari. 
Baba Wema Sepetu amewahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mnamo miaka ya 1970 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Kambarag Nyerere.  Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere.
Na March 27 2013 Balozi Sepetu aliteuliwa na Rais wa Zanzibar, Dr Mohammed Shein,  kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitegauchumi ya Zanzibar (ZIPA).
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho Ya Marehemu Mahali Pema peponi.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...